GREATER MANCHESTER POLICE
Picha za CCTV zinazomuonyesha Salman Abedi usiku aliofanya shambulizi katika ukumbi wa Manchester na kuwaua watu 22 zimetolewa.
Maeneo 14 yanasakwa na wanaume 11 wamekamtwa kwa kushukiwa kuhusika katika ugaidi.
- Shambulizi la Manchester: Tunafahamu nini?
Abedi alitambuliwa saa mbili baada ya shambulizi la siku ya Jumatatu.
Waziri mkiu Theresa May anasema kuwa kiwango cha tisho lililopo kimepunguzwa na wanajehsi waliotumwa kuwasaidia polisi wataondolewa kuanzia siku ya Jumatatu
GETTY IMAGES
Mamia ya polisi waliojihami wanaendelea kulinda mamia ya tamasha kote nchini Uingereza.
Mamia ya polisi walitumwa wakati mashabiki 50,000 walihudhuriw tamasha la Courteeners kwenye uwanja wa kriketi wa Old Trafford, ambalo ni tamasha kubwa kufanyika mjini humo tangu shambulizi kutokea.
- Mshukiwa wa shambulio la Manchester atajwa
Ulinzi zaidi umewekwa leo wakati wa mbio za Great Manchester Run ambapo maelfu ya wanariadha wanatarajiwa kushirikia
GETTY IMAGES
Comments
Post a Comment