Zaidi ya Tembo 40 wauawa DRC, mwaka huu

Idadi kubwa ya tembo huuawa na majangiliHaki miliki ya picha
mage captionIdadi kubwa ya tembo huuawa na majangili
Maafisa kutoka Hifadhi ya Taifa ya Garamba nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamesema kuwa Tembo 45 wameuawa tangu mwanzo wa mwaka huu.
Maafisa hao wanasema endapo uhalifu huo utaendelea kukithiri, Tembo huenda wakapotea kabisa katika mbuga hiyo, ambayo ni moja ya maeneo yaliyo na tembo wengi zaidi barani afrika.
Ripoti zinasema Ndovu hao huuawa na makundi ya waasi nchini DRC, wapiganaji wa kundi la waasi wa LRA kutoka Uganda, na waasi wa Sudan Kusini.

Comments